Google PlusRSS FeedEmail

LUGHA ZA MATUSI ZAMPONZA EMINEM, AZUILIWA KUFANYA SHOW NCHINI UINGEREZA

Ripoti zilizoandikwa na gazeti la The Daily Mirror zinaeleza kuwa lugha ya matusi kwenye nyimbo za Eminem ndio chanzo cha yeye kukataliwa kufanya show kwenye eneo la Hyde Park, Uingereza.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mmiliki wa Hyde Park, Linda Lennon ameeleza kuwa aliamua kutompa nafasi Eminem kuperform katika eneo hilo kwa kuhofia ujumbe wa nyimbo zke na lugha anayotumia ingewaudhi wateja wake.

Ofisi ya Mayor wa jiji la London, Boris Johnson imeeleza kuwa haikuhusishwa kabisa katika uamuzi wa kumzuia Eminem kuperform katika Hyde Park. Walifafanua kuwa hawakufahamu Eminem ni nani na hawakuwa na uwezo wa kuingilia maamuzi ya Wamiliki wa eneo hilo.

Eminen alitarajiwa kuperform katika Hyde Park June 3 kabla hajazuiwa.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging