Google PlusRSS FeedEmail

LUPITA NA PHARREL WILLIAMS WACHAGULIWA KUINGIA KATIKA ACADEMY

LUPITA Nyong’o anazidi kuwaongezea wakenya nafasi ya kutajwa kwenye tuzo za Oscar hata kama sio katika kupata tuzo tu baada ya kuongezwa kuwa kati ya watu 271 wanaounda Academy ya tuzo za Oscar mwaka huu.

Muigizaji huyo wa 12 Years A Slave, ambaye ni mshindi wa tuzo ya Oscar ya mwaka jana kama muigizaji bora wa kike msaidizi, anaungana na wasanii wengine waliong’ara mwaka jana katika tasnia ya filamu pamoja na mwanamuziki Pharrell Williams kama members wapya wa Academy hiyo.

Wasanii wengine wenye umri mdogo watakaoungana na Lupita ni pamoja na Josh Hutcherson, Michael Fassbender, Ben Foster, Sally Hawakins, Julia Lousi-Dreyfus, Chris Rock na Jason Statham.

Rais wa Oscar Academy, Cheryl Boone Isaac ameeleza kuwa Academy ya mwaka huu itawahusisha watu ambao wana vipaji zaidi na wabunifu katika masuala ya fulamu.

“Mchango wao katika filamu umewaburudisha hadhira kote duniani, na tunajivunia kuwakaribisha kwenye Academy.” Aliseam Cheryl Boone.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging