Google PlusRSS FeedEmail

MAVAZI YAMEMPONZA JAY-Z

Uchaguzi wa mavazi unahitaji umakini wa hali ya juu la sivyo wanaojua mavazi wanaweza kukuumbua wakati unadunda kama tenesi mtaani.

Mr Hov, Jay Z ameripotiwa kuwa alikutwa mitaa ya jiji la New York akiwa amevaa jezi (Jersey) ya mpira wa miguu ya Rodarte ambayo ilitengenezwa maalu kwa wanawake yenye namba 5 kubwa kwa mbele.

Kutokana na hatua hiyo, watu wameendelea kujiuliza kama Jay Z alikuwa amevaa jezi ya Beyonce mke wake kuonesha upendo, au alinunua nguo hiyo makusudi.

Jay Z na mke wake Beyonce huvaa mavazi ya Rodarte, na Jumapili iliyopita wawili hao waliwasili New York na Beyonce alikuwa amevaa sweta la Rodarte likiwa limeandiwa Radarte.

Inaelezwa kuwa hata miaka ya nyuma kwenye video za nyimbo za Jay Z alikuwa akitupia jezi za kike ila watu walikuwa hawafuatilii kwa umakini!

Kabla hujabisha au kulibali, pitiapitia video za nyimbo za Jay Z za miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging