Google PlusRSS FeedEmail

NANDO - "LULU AKIKUBALI NIPO TAYARI KUMUOA"


MSANII wa filamu nchini Lulu, pamoja na mwakilishi wa shindano la Big, Brother Ammy Nando walijikuta wakitengeneza vichwa vya habari wakihusishwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi ambapo hata hivyo wawili hao walijikuta wakiuelezea uhusiano wao kuwa ni kirafiki zaidi.

Ingawa wawili hao wamekuwa na majibu sawa ya kudai kuwa wanaurafiki wa kawaida tu, Nando amekuwa akimuangalia Lulu kwa jicho la pembeni kama ‘wife material’.

Mwakilishi huyo wa shindano la Big Brother, Nando kwa kupitia mahojiano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, alieleza kuwa anavutiwa sana na msichana huyo kwa kuwa ni mtafutaji wa pesa japo anaumri mdogo.

“Lulu ni mwanaharakati, ni mdogo lakini she knows how to get money.” Amesema Nando.

Aongeza kuwa kutokana na sifa alizonazo za kutafuta pesa pamoja na uzuri wake, atakapokuwa na mpango wa kuolewa yeye yuko tayari kutulia nae.

Hivi karibuni Lulu alisema kuwa hana uhusiano wa mapenzi na Nando na ana mpenzi wake mwingine.

Nando pia alieleza uhusiano wake na Dayna Nyange na kudai kuwa ni rafiki yake tu na wanashirikiana katika video ya wimbo wake mpya, “nitauza sura mle ndani.”

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging