Google PlusRSS FeedEmail

DIAMOND PLATINUM AZUNGUMZIA TUHUMA ZA WIZI WA NYIMBOHIVI Karibu kumeripotiwa baadhi ya wasanii wakitoa malalamiko yao juu ya kuibiwa nyimbo au mawazo ya nyimbo zao na baadhi ya wasanii wakubwa.

Mbali na hayo malalamiko kutolewa wapo baadhi ya wasanii kulalamika kuibiwa nyimbo na mawazo yao na msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini,Diamond Platinumz, ambapo madai hayo huzua hisia tofauti kwa watu wengi.

Hivi karibuni, mshiriki wa BSS Wababa naye alijitokeza na kudai kuwa Diamond amemuibia wimbo wake wa Kitorondo na kwamba baadae aliubadilisha jina na kuuita MdogoMdogo.

Kutokana na malalamiko hayo hivi karibuni msanii huyo Diamond amezitolea majibu tuhuma hizo wakati akifanya mahojiano maalumu katika kipindi cha redio kilichopo jijini Dar es Salaam.

Diamond aliweka wazi kuwa hayo ni madhara yanayotokana na ukubwa wa muziki aliokuwa nayo hali inayopelekea baadhi ya watu na hata wasanii kumzungumzia vitu ambavyo si vya maana kwake.

“Unapokuwa mkubwa sana kunakuwa kuna faida yake na madhara yake. Na madhara yake yalivyo, unapokuwa mkubwa sana kitu ambacho hakina maana watu wanajaribu kukifanya kuwa na maana, either kionekane kizuri au kibaya.”Alisema Diamond.

Diamond alifafanua kuwa alipotoa wimbo unaojulikana kwa jina la moyo wangu nyimbo nyingi sana zilitoka zinaitwa Moyo wangu, lakini hakusikika akilalamika mtu kumuibia wimbo huo, kwani alikuwa akitambua kuwa hilo ni neno kwani hakuna mwenye neon lake duniani.

Akizungumzia tuhuma zilizotolewa na msanii Wababa hivi karibuni kuwa alimuibia wimbo wake wa Kitorondo na baadae akaubadili kuwa Mdogo Mdogo, Diamond amesema huo ni wimbo wa Asili ambao ulikuwa unaimbwa na bendi ya Tandale Modern Taarabu, na pia ni ngoma ya mdundiko wa zamani.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging