Google PlusRSS FeedEmail

PIGO JINGINE KWA WASANII WA FILAMU 'MZEE SMALL AFARIKI DUNIA

                                         

Muigizaji mkongwe hapa nchini, Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small amefariki dunia usiku wa leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Akithibitisha taarifa ya kifo cha Mzee Small, mwanae aitwae Mahmoud amesema mzee wake amefikwa na mauti hayo majira ya saa nne usiku wakati akiwa hospitalini hapo akiendelea kupatiwa matibabu.
Mipango inafanyika nyumbani kwao Tabata na kadri taarifa zitakavyokuwa zikitufikia tutaendelea kujulishana.

                            
Ni pigo lingine tena kwenye tasnia ya sanaa baada ya kuondokewa na wasanii na kadhaa majuma yaliyopita.


-Amin.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging