Google PlusRSS FeedEmail

WEBA ABEBA UJAWEPESI..

                      
Hayawi hayawi hatimae yamekuwa  Wema Sepetu sasa ni mjamzito. Baada ya misukosuko ya muda mrefu ikiwemo kuporwa na wasichana wenzake penzi lake la Diamond, sasa Wema amepata kile alichokuwa akikililia kwa muda mrefu.

Chanzo cha habari hii kutoka kwa marafiki wa Diamond kimedai kuwa Wema amenasa ujauzito na kugundulika hivyo walipokuwa Afrika Kusini kwenye tuzo za MTV-MAMA na kumfanya Diamond achanganyikiwe kwa furaha.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, inadaiwa kuwa Diamond kwa sasa kawa kama mtu aliyepagawa kwa furaha kutokana na taarifa hizo njema na tayari ameshaanza maandalizi ya kijacho chake.

Kugundulika kwa ujauzito wa Wema ni baada ya kuanza kujisikia vibaya walipokuwa Afrika Kusini ikiwemo kichefuchefu na kizunguzungu alipokuwa hotelini alipofikia na kulazimika kwenda hospitali kwa uchunguzi zaidi..

Inasemekana kuwa Wema alisindikizwa na Aunt Ezekiel kwenda hospitalini waliyekuwa naye huko Afrika Kusini kumpa sapoti Diamond na madaktari ndiyo waliomjuza kuwa anakiumbe tumboni cha wiki 7...

Taarifa za madaktari hao zilimfanya Wema awe kama mwehu aliyepagawa na kurudi hotelini kwa mumewe Diamond huku akiwa na tabasamu ambalo hapo awali Diamond hakuwahi kuliona....

Inasemekana kuwa mpaka sasa siyo Diamond wala Wema aliyewaambia wazazi wake kuhusiana na mimba hiyo zaidi ya watu wa karibu wa wawili hao waliowasindikiza Afrika Kusini.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging