Google PlusRSS FeedEmail

MUIMBAJI WA SUMU YA TEJA ATEMBEA KWA MIGUU DAR, MORO

MUZIKI  ni chombo kikubwa kinachoweza kuleta mapinduzi endapo kitatumiwa ipasavyo katika jamii.

Vitalis Maembe, anaefahamika zaidi kwa wimbo wake wa Sumu ya Teja ameanza harakati za kutetea haki za watoto wa Afrika ikiwa ni siku mbili kabla ya kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika (June 16).

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Vitalis alisema kuwa anatembea kwa miguu kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ili kuhamasisha watu mbalimbali pamoja na serikali kuzingatia haki ya mtoto.

Amesema ametembelea gereza la watoto na pia kukutana na wadau mbalimbali kabla hajaanza safari hiyo ambayo inamkutanisha na watu wengi zaidi na kufikisha kilio chao.

“Katika kutembea kwangu, pia nakusanya maoni ya watu wanasemaje juu ya suala hilo. Na mpaka kufikia sasa hivi watu wanataka kusikia kauli kutoka kwa wahusika serikalini hasa waziri wa Elimu na waziri anaehusiana na masuala ya watoto na jamii."

 Anasemaje kuhusu elimu kwa watoto wasiojiweza au watoto ambao wana migogoro ya kisheria au watoto ambao wameacha shule, je anatoa kauli gani kuhusu hilo.

“Halafu pili kuhusiana na vibanda vya video ambavyo viko mitaani vingi tu ambavyo vinaelekeea kuharibu maadili ya watoto ambavyo vibanda hivyo wateja wakubwa ni watoto, Sasa na wafanyabiashara wa vibanda hivyo wanajitahidi kubadilisha kila namna ya kuweza kuweka mvuto kwa watoto na hizo namna ziko kinyume na maadili.”

Amesema anafurahi kuona kuna watu wanajiunga nae kwa matembezi hadi sehemu fulani kisha wanaendelea na shughuli zao na kwamba kila wanapokutana huwaimbia nyimbo za kijamii na baadae hujadili masuala muhimu.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging