Google PlusRSS FeedEmail

BANZA STONE AJIUNGA EXTRABONGO

Mwimbaji mkongwe wa muziki wa dansi aliyekumbwa na misukosuko mingi ya kiafya kwa kipindi kirefu, Banza Stone amerejea rasmi katika bendi ya Extra Bongo tayari kwa kupiga kazi kama zamani.

Banza alianza kuonekana akiimba na bendi ya Extra Bongo tangu February mwaka huu.

Kiongozi wa bendi hiyo inayomilikiwa na Chief Kiumbe, Ali Choki amethibitisha taarifa hizo wakati akiongea na TBC1 na kueleza kuwa bendi hiyo imepanga kufanya ziara nchi nzima.

Katika hatua nyingine Ali Choki amesema kufuatia ushindani uliopo kwenye tasnia ya muziki kati ya muziki wa Bongo Flava na Muziki wa dansi, ameamua kufupisha urefu wa nyimbo zake ili kukabiliana na changamoto hiyo.

Amesema kwa kawaida nyimbo za dansi huwa na dakika 8 hadi 12 wakati nyimbo za bongo flava zina dakika kati ya 3 hadi 5.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging