Google PlusRSS FeedEmail

MBASHA ASOMEWA MASHTAKA 4 AKUBALI 2




KESI ya ubakaji inayomkabili mwimbaji maarufu wa nyimbo za injiri Emmanuel Mbasha (32), imetajwa tena leo katika mahakama ya wilaya ya Ilala ambapo muimbaji huyo amesomewa tena mashataka yake yake huku akikubali hoja mbili kati ya nne zilizosomwa kwenye mashtaka hayo.

Akisoma hoja hizo mbele ya hakimu Wilbert Luago mwendesha mashtaka wa serikali Nasoro Katunga alisema mnamo tarehe 23 Mei mwaka huu mtuhumiwa alimbaka binti aitwaye Yerusalemu Boazi (17), na kumlazimisha asimwambie mtu yoyote.

Katunga alisema wakati akitenda kosa hilo mke wake Frola Mbasha hakuwepo nyumbani na kudai kuwa Mbasha na huyo binti walibaki wao tu pale nyumbani kwao maeneo ya Tabata.

Katunga aliendelea kufafanua kuwa mnamo Mei 25 mwaka huu Mbasha alirudia tena kitendo kitendo cha ubakaji baada ya kumuomba binti huyo amsindikize waende kumtafuta mke wake ambaye hakuwepo nyumbani na walipofika maneo ya Tabata Mbasha alimbaka tena binti huyo.

Alisema tukio hilo la ubakaji lililipotiwa katika kituo cha polisi Tabata na Boazi alipewa PF3, kwa ajili ya kupata matibabu na uchunguzi uliofanywa ulibaini kuwa ni kweli binti huyo aliingilia kimwili.

Katika kesi hiyo ambayo Mbasha anatetewa na wakili aitwaye Mathew Kakamba, Mbasha alikubali na kukataa hoja mbili zilizosomwa katika shtaka hilo ambapo alisema ni kweli Mei 23 mke wake Frola Mbasha hakuwepo nyumbani lakini hakutenda kitendo hicho cha ubakaji .

Katika shtaka lingine ambapo inadaiwa alimbaka binti huyo maeneo ya Tabata Mbasha alisema ni kweli alimuomba binti huyo amsindikize kumtafuta mke wake ambaye hakuwepo nyumbani lakini hakumbaka.

Baada ya kusomewa mashataka hayo na muendesha mashataka wa serikali, Jaji Luago alihailisha kesi hiyo hadi Agosti 22 mwaka huu baada ya wakili anayemtetea Mbasha kudai atakuwa na safari kwa siku za hivi karibuni nje ya Mkoa .

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging