Google PlusRSS FeedEmail

JAY Z ATOKWA NA MACHOZI

Kuna wakati wasanii hufanya ubunifu na kutengeneza picha ya maneno ya kufikirika ama kutumia mfano wa kinachoendelea kuandika nyimbo zao, lakini huwa na hisia kali zaidi pale wanapoandika ukweli wa maisha yao.

Uandishi wa verse ya Jay Z katika wimbo wa Young Jeezy ‘Seen It All’ iliyobeba ukweli wa maisha yao ya zamani ulipelekea rapper huyo kutokwa machozi wakati akichora mistari.

Young Jeezy ameiambia MTV kuwa alipigiwa simu na Jay Z ambaye alimueleza kilichojili wakati anaandika wimbo huo.

“Tulikuwa tunazungumza kwa simu na Jay Z na alisema, ‘Yo, Jeezy, nilipokuwa naandika verse nilikuwa na machozi machoni’, ni kwasababu ilimkumbusha mbalis sana ‘back to Marcy’.” Alisema Young Jeezy.

“Kila kipande katika wimbo huo kilikuwa halisi…naweka mkono wangu kwenye Biblia.” Alisisitiza.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging