David Banner na Linah walikutana studio na watayarishaji wengine akiwemo P-Funk Majani, Lamar, Nahreel na Ematheboy na kwa pamoja watayarishaji hao walitengeneza mdundo.
Akiongea na Bongo5, Lamar ameeleza baada ya kufanya mdundo David Banner aliingiza sauti na baadae Linah akaweka chorus na imebaki verse.
“Sisi tulikutana tu tukaanza kutengeneza beats, tumekata samples pale tukaanza kushauriana tufanye vipi, halafu akaingiza sauti David Banner kama chance tu na Linah akaingiza chorus ikawa bado kuingiza verse, yaani tulikuwa tunafanya vitu kwa pamoja, tunatengeneza beat kwa pamoja. Project ambayo amefanya Linah na David Banner itaendelea tunafinalize.” Amesema Lamar.








