Google PlusRSS FeedEmail

'MATUSI' YAMSABABISHA DAYNA KUACHA KUJICHUBUAMSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Dayna Nyange, ajikuta akikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo lugha mbaya kutoka kwa baadhi ya mashabiki zake kwa sababu ya kitendo alichokifanya cha kujibadilisha rangi ya ngozi yake ‘kujichubua’.

Hali hiyo imeibuka hivi karibuni baada ya msanii huyo kuamua kujibadilisha rangi yha ngozi yake kwa kujichubua na kuonekana tofauti kwa kuwa mweupe mwili mzima tofauti na awali alivyozoeleka kuonekana.

Kutokana na maneno ambayo yamemuandama msanii huyo kutoka kwa mashabiki zake juu ya kutumia mkologo, msanii huyo ameamua kupunguza kutumia mkologo huo, ingawa siyo kama ameacha kabisa

Akizungumza jijini Dar es Salaama katika mahojiano maalumu, Akiongea katika, Dayna ameeleza kuwa amekuwa akikosolewa na watu wengi huku wengine wakitumia lugha mbaya dhidi yake lakini yeye ameipokea vizuri kwa kuwa anaamini ni watu wanaompenda, hali iliyompelekea kuamua kupunguza kutumia mkologo huo.

“Ni sawa kwa sababu mimi naamini ni watu wangu wa karibu na ni watu ambao wananipenda ndio maana wanakuwa wanasema japo wengine wanatumia kauli mbaya. Lakini pia ni sawa kwa sababu mimi najua hao ni binadamu na kila binadamu anajua jinsi ya uwasilishwaji kwa mtu vile ambavyo anajisikia kwa hiyo ni mimi kutumia tu akili nakipokeaje.” Amesema Dayna Nyange.

Ameeleza kuwa yeye anaamini hakuna kitu ambacho aliwahi kukifanya kabla kikawa gumzo au tatizo kwa watu na ndio maana watu wanaamua kulichukulia hili kama tatizo kubwa.

Mwimbaji huyo alitangaza uamuzi aliouchukua kufuatia changamoto hizo alizokutana nazo ingawa anaamini kila mtu anauhuru wa kufanya maamuzi kama alivyoamua yeye.

“Kwa hiyo mimi naweza kusema ni sawa, inawezekana kweli nimekosa. Lakini mimi kama binadamu pia nina maamuzi yangu na nina sababu nyingi tu za kufanya kile ninachokifanya. Japo nimesikia maneno mengi sana mpaka Lol..’nimeacha.!

“Siwezi kusema kuwa nimeacha kabisa lakini nimetoka kule nilikokuwa, sasa hivi narudi kuwa Dayna yule ambaye mnataka awe. Japo pia binadamu pia mnakitu kimoja, sifieni kile kilicho bora kabla hakijakuwa sio.” Ameaongeza.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging