Google PlusRSS FeedEmail

TERRENCE JENKINS KUIBA UJUZI WA WASANII WA TANZANIA

Mtangazaji, muigizaji na mwandishi wa vitabu kutoka Marekani Terrence Jenkins ambaye ameletwa nchini na mheshimiwa rais Jakaya Kikwete, anathamini kile ambacho wasanii wa Tanzania wanacho na anakihitaji sana pamoja na kwamba amekuja kwa lengo la kuwapa/ kufundisha na kushare uzoefu alionao katika kiwanda cha sanaa ya kimataifa.

Terrence J ambaye ameongozana na Chaka Zulu (Meneja wa wasanii na mmoja wa waanzilishi wa lebel ya DTP ya Ludacris), David Banner (rapper na Producer na Muigizaji) na Riva Shalton (Mfanyabiashara Mkubwa katika sanaa) ameeleza uhitaji wao wa kubadilishana maarifa na wasanii wa Tanzania alipokuwa anafanya mahojiano maalumu nchini.

“Nahisi kama nina mengi ya kujifunza nitakaporudi. Nimekuwa nyumbani, ni uzoefu mzuri na nataka kujifunza. Watu wengi wanasema wanataka kujifunza kutoka kwetu lakini tumekuja kujifunza kutoka kwenu pia.” Alisema Terrence J.

“Nadhani nchi yenu ina ‘turning point’ nzuri na ya kuvutia (kuifahamu) na wasanii wa hapa ni wazuri wa kushangaza sana na wana mzuka sana. Na sisi tunadhani ni vitu ambavyo tunaweza kuvifyonza na tukarudi nyumbani tukiwa bora zaidi.” Amesema Star huyo wa Think Like A Man Too na mtangazaji wa E! Entertainment.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging