Google PlusRSS FeedEmail

MCHUMBA WA CHRIS BROWN AELEZEA CHANGAMOTO ANAZOKUMBANA NAZOGirlfriend wa Chris Brown, Karrueche Tran ambaye hivi mapenzi yake na mwimbaji huyo yamekuwa ya kuachana na kurudiana mara kwa mara, ameelezea changamoto anazokutana nazo kwa kuwa na mtu aliyekuwa mpenzi wa Rihanna mwenye mashabiki wengi duniani.

Akiongea na Just Keke, Karrueche ameeleza kuwa kutokana na umaarufu wa Rihanna ambao anaamini ni maarufu zaidi ya Chris Brown, amekuwa katika vita na mashabiki zaidi ya milioni 14 wa Rihanna.

“Katika hali hii boyfriend wangu ni mtu maarufu ambaye mpenzi wake wa zamani ni maarufu hata zaidi yake… kwa hiyo, sio tu kama napambana na yeye tu (Rihanna), napambana na mashabiki wake milioni 14 au vinginevyo.” Alisema Karrueche.

“Hebu vuta taswira, najisikiaje pale napoingia Twitter na kutakana na mambo yote …wanafanya kila kitu cha ajabu (crazy) na ni kama hawafahamu chochote kuhusu mimi.”Aliongeza.

Mrembo huyo alisisitiza kuwa amejaribu kuwa na mtazamo chanya katikati ya mapenzi hayo ya pembe tatu (Chris Brown, yeye na Rihanna) lakini amekiri kuwa inamuwia vigumu sana.


This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging