Google PlusRSS FeedEmail

MWANAMKE ATUMIA ZAIDI YA MILIONI 49 AFANANE NA KIM KARDASHIAN

Kupenda ama kutamani kuwa kama star fulani unaemkubali hakuna sheria ya mipaka zaidi ya mwenyewe kuthibiti hisia zako zisipitilize, lakini wapo wengine ambao wamechoka kutamani kuwa kama fulani na wameamua kutumia nguvu kuwa kama yeye.

Claire Leeson, msichana mwenye umri wa miaka 24, mkaazi wa Landani ametumia zaidi ya $30,000 (Tsh 49,755000)kufanya upasuaji ili afanane na Kim Kardashian.

Claire ameiambia This Morning kuwa aliamua kufanya hivyo kwa sababu alipokuwa shuleni wenzake walikuwa wanamcheka na kuuita ‘mbaya’ kuliko kitu chochote kilicho hai.

“Nilikuwa naambiwa kila siku mimi ndiye mbaya kuliko kitu chochote kilicho hai na kwamba inabidi nijiue. Nilipoacha shule marafiki zangu waliniambia kuwa ninavitu ambavyo vinafanana na Kim Kardashian.” Amesema Claire.

Ameeleza kuwa baada ya kuambiwa hivyo na marafiki zake aliamua kuanza kuangalia kwa makini Keeping Up With The Kardashians na akagundua kuwa kweli kuna vitu ambavyo wanafanana na Kim Kardashian.

“Tunafanana katika mabishano na vitu vingine. Nikafikiri ni mzuri sana na kwa kweli nilitaka kufanana nae.”

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging