Google PlusRSS FeedEmail

SELENA GOMEZ AWAJIBU MASHABIKI WAKE

Wasanii wakubwa hupata likes na comments nyingi kutoka kwa mashabiki wao kwenye mitandao ya kijamii kiasi cha wengi kufikiria kwamba huenda huwa hawazisomi comments. Lakini mwimbaji na muigizaji maarufu wa kike Selena Gomez ameonesha kuwa hufuatilia comments za mashabiki wake.

Kupitia Instagram, Selena amemjibu shabiki wa kike ambaye aliandika comment ya kumuombea afe kwa ugonjwa wa saratani, akaunti ambayo ilikuwa deactivated muda mfupi baada ya kupata jibu la busara la Selema Gomez.

Comment ya Selena ilimueleza msichana huyo jinsi ambavyo hakupenda kile alichoandika kama msichana mdogo na kueleza kuwa yeye amepitia hayo na mashabiki na familia.

Alimshauri kuwa unaweza kuwa haumpendi mtu lakini kumuombea kitu ambacho kinaweza kutokea kwako ama kwa familia yako hakukubaliki. Zaidi alimuomba ajifunze zaidi huku akimoumbea abarikiwe. Tofauti na maelezo ya shabiki huyo, selena alimsifu kuwa ni mwanamke mzuri.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging