Google PlusRSS FeedEmail

TERRENCE J WATOA SEMINA KWA WASANII WA BONGO







Ile ahadi aliyoiahidi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete leo imetimia baada ya wasanii mbalimbali wa filamu na waimbaji wa muziki kutoka kwenye aina tofauti ya muziki ikiwemo waimbaji wa Bendi,nyimbo za Injili na Bongo Fleva.

Terrence J,Chaka Zulu na David Banner ndio walikua waongozaji wa semina hiyo ambayo ilianza saa 4 asubuhi na kumalizika jioni saa 11 na nusu July 14,miongoni mwa wasanii waliiopata nafasi ya kuongelea changamoto za muziki wa Tanzania ni pamoja na Khadija Kopa.

Khadija Kopa amesema muziki wa Tanzania una changamoto nyingi na kusema ili kuwe na mafanikio kwenye sanaa yetu ya Tanzania kuna umuhimu wa wasanii wote kuwa na umoja ndipo mengine yatafuata na kuwa rahisi.

Wadau hao wamekuja nchini kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa muziki na filamu ili kuweza kujiingizia kipato kupitia kazi zao na kujitangaza zaidi kimataifa,semina hii imefanyika kwenye ukumbi wa BOT uliopo Posta Dar es salaam.














This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging