Ukoo wa Okoye umeendeleza mbio za kupokezana vijiti kwenye suala zima la kufunga ndoa, kwani baada ya Peter kuvuta jiko na kisha kufuatiwa na Paul alafu kaka yao mkubwa Jude, hatimaye dada yao mpendwa aitwaye Mary Okoye amefuata nyayo za kaka zake baada ya kufunga pingu za maisha na muigizaji nyota wa Nollywood anayefahamika kwa jina la Emma Emordi.
Ndoa ya wawili hao ilifungwa katika eneo la Asaba mjini Delta nchini Nigeria wikiendi iliyopita na kuhudhuriwa na baadhi ya mastaa wakiwemo Psquare wenyewe walioongozana na wake zao Anita na Lola. Tazama picha zaidi hapo chini.