Google PlusRSS FeedEmail

KUNANI ORIJINO KOMEDI

                                 
Hakuna ubishi kuwa miaka michache iliyopita kundi la Orijino Komedi ndilo lenye mashabiki wengi hapa nchini.

Ilikuwa ukifika muda wa kurushwa kipindi kila mtu alikuwa hang'ooki Katika TV yake hata foleni barabarani zilikuwa zinapungua watu huwa wamejibanza popote penye TV ili kuona kipindi cha siku hiyo.

Umaarufu wao uliongezeka zaidi pale walipohama EATV na kuhamia TBC.

Umaarufu wao uliendelea kuwepo hadi siku za karibuni ambapo ulishuka kwa kasi sana, taarifa ambazo  tumezipata ni kuwa kwa sasa kundi hilo limevunjika na kila mtu anafanya  kazi kivyake.

Chanzo chetu kutoka kituo cha TV walichokuwa wakifanya kazi kinasema kuwa kwa sasa kila mtu ana hamsini zake na hawafanyikazi tena pamoja.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging