Google PlusRSS FeedEmail

DIAMOND ATUMIA FUMBO KUFIKISHA UJUMBE

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Diamond Platnum, ameamua kutoa ya moyoni kwa kutoa ushauri kwa baadhi ya marafiki wanaomzunguka kupitia account yake ya Instagram ambapo aliandika kuwa kama mnamapenzi ya dhati kwa msanii wenu mngemshauri apunguze marafiki wanaoendekeza starehe.

 “Nafkiri ningewaona kweli Mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa Msanii wenu  kama mngemshauri apunguze Mashoga wapenda anasa na apunguze Stareh zisizo na Faida, wenda ingemsaidia Pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe.

Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha Mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi. Waswahili wanasema Mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka Ng’ombe wake Kwenye Maji safi ila yeye ng’ombe mwenyewe ndio anatakiwa aamue kunywa maji!!!!!

Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie ???? Nisiende Studio nikae dukani nimuuzie mie????.. ni juhudi zako kwanza!… leo hii mimi Hata ningepewa Mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo wa mie mwenyewe kwanza kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu nisingefikia hapa nilipo!….Mxieeeeeeeew!�� Kama nimekuchefua Lamba ndimu Usitapike”.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging