Google PlusRSS FeedEmail

DIAMOND ABEBA TENA TUZO ZA TTM

DIAMOND anazidi kujiweka katika sehemu nzuri juu ya kukuza muziki wake ambapo CV yake katika muziki inazidi kupanda na mwaka huu unaweza kutajwa kuwa mwaka wa tuzo kwa mwimbaji huyo ambaye amevuka mipaka na kuzinyakua au hata kutajwa tu kuziwania.

Wimbo wa My Number One wa Diamond umeshinda tuzo ya Wimbo Bora wa Afrika Mashariki katika tuzo za Burundi zinazojukana kama TTM Awards.

“Asante sana kwa Media wadau na Mashabiki zangu pendwa kwa kuifanya Number One kuwa Nyimbo Bora ya East Africa ya Mwaka kwenye tunzo za #TTMAwards nchini Burundi.....” Ameandika Diamond kwenye Instagram akiambatanisha na picha ya mtu aliyempokelea tuzo hiyo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging