Google PlusRSS FeedEmail

JE UNATAKA KUWA NYOTA WA TAMTHILIA NA FILAMU?

                                                  Mshindo Jumanne
Kampuni maarufu ya filamu ya Safina Movies imeandaa nafasi za bure kabisa kwa msanii yoyote mwenye kipaji kujiunga na kampuni hiyo kwa ajili ya kuonyesha kipaji chake, msanii chipukizi atakayejiunga na kundi hilo atafundishwa na kushiriki katika kazi za kampuni hiyo.

Akiongea na wanahabari mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Mshindo Jumanne amesema kuwa kampuni hiyo imekusudia kukuza vipaji vya wasanii chipukizi waliokosa fursa hiyo pamoja na kuwa na uwezo wa kuigiza kwa vitendo na si maneno.

“Wasanii wenye vipaji ni wengi sana mitaani lakini hawapewi fursa kuigiza na kushiriki katika filamu na tamthilia, ndio maana kampuni yetu ya Safina Movies imeliona hilo na kuwapa nafasi za kuonyesha vipaji vyao bila gharama,”anasema Mshindo.

Mkurugenzi huyo amedai kuwa kutokana na ugumu wa ajira nchini Tanzania baadhi ya wasanii chipukizi wamejikuta wakitapeliwa kwa kuchangishwa fedha na kuuziwa fomu kwa gharama kubwa na kuishia kupigwa picha bila kupewa kazi.

Aidha kampuni ya Safina Movie yenye maskani yake Kijichi Mbagala inasajili wanaohitaji kuwa wasanii nyota Bure kabisa kama msanii anahitaji anaweza kuwasiliana na uongozi kwa namba hizi 0658 010 100/ 0752 132 347 utakuwa umeingia katika tasnia ya filamu.

Safina movie inahitaji wasanii zaidi ya 400 kwa ajili ya tamthilia inatayorushwa katika moja ya televisheni kubwa za Afrika Mashariki, kampuni hiyo ambayo ni watengenezaji na wasambazaji wa filamu nchini imesema pia wasanii hao pia watashiriki katika filamu za kampuni hiyo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging