Google PlusRSS FeedEmail

KASSIM MGANGA AMZUNGUMZIA ALI KIBAMwimbaji kutoka Tanga, ‘Tajiri wa Mahaba’ Kassim Mganga amemtaja Ali Kiba kuwa ndiye msanii wa bongo flava anaemkubali zaidi Tanzania.

Ali Kiba amefunguka katika mahojiano maalum aliyofanya na tovuti ya Times Fm na kueleza kuwa mbali na kuwa ni mwimbaji mwenye uwezo mkubwa, hata kitabia yuko vizuri.

“Ali Kiba (ndiye my favorite artist in TZ), mimi binafsi nampokea vizuri sana. Nafikiri anachokifanya mimi kinanivutia sana. Napenda uandishi wake, napenda melodies zake na napenda utulivu wake. Ana hekima kama zangu, yuko kimyaa (anacheka).” Kassim ameiambia tovuti ya Times Fm.

Kassim Mganga ameeleza kuwa mwaka jana kabla hajatoa wimbo wake ‘I Love You’ uliokuwa hit, alikuwa na mpango wa kufanya wimbo na Ali Kiba na walikuwa tayari wamekubaliana lakini mambo yaliingiliana na kazi haikukamilika.

Katika hatua nyingine, Kassim Mganga ameeleza kuwa watanzania hatupaswi kuendekeza majigambo na uadui kati ya wasanii badala yake kufanya kazi na kuwasapoti wale ambao wanaiwakilisha nchi yetu katika mataifa mbalimbali kama vile Diamond badala ya kuwajengea uadui.

“Diamond ni mtu ambaye ameweza kutufungulia sana soko letu kiukweli, tunashukuru. Tunatakiwa kuwa nyuma yake tumsapoti tuendelee kumsukuma na sisi huku tunaendelea kujongea. Kwa hivyo, vinapokuwa vinajengwa vitu kama hivyo (uadui/majigambo) sio jambo zuri kwa sababu vinajenga uadui na mwisho wa siku muziki tunakuwa tunaufanya kimajigambo tu lakini sio kwa ajili ya kuutangaza muziki wetu…”

SOURCE:TIMESFM

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging