Google PlusRSS FeedEmail

PASTOR MYAMBA KUFUNGUA KAMPUNI KWA ZAWADI YA KITITA CHA MILIONI 250


MSANII na muongozaji wa filamu nchini Pastor Myamba afunda ndoa jana katika visiwa vya Zanzibar, huku akiwa amepewa zawadi nono zinazoweza kumsababisha akafungua kampuni yake mpya au kuendesha biashara yoyote.

Msanii huyo ambaye amefunga ndoa  iliyohudhuriwa na mastaa mbalimbali katika visiwa vya Zanzibar, alizawadiwa kitita cha fedha pamoja na gari ya kifahali hali hiyo imeonesha kuwa ndio msanii wa kwanza nchini kufunga ndoa na kuzawadiwa zawadi kubwa.

Kwa mujibu wa msanii JB alieleza kuwa msanii huyo na mkewe wamezawadiwa zawadi mbalimbali ikiwemo kitita cha milioni 250, na gari la jipya hali hiyo inaonesha kuwa wanauwezo wa kufungua kampuni yao nyingine hata kama ya uigizaji.

Kupitia account ya Instagram ya msanii JB alituma picha iliyoonesha zawadi ya kitita cha fedha alizozawadiwa huku akiwa ameambatana na baadhi ya wasanii wakongwe wa bongo movi.

“Taarifa ni kwamba pesa hizo hii ni moja ya zawadi alizopewa Pastor Myamba pamoja na mke wake baada ya kufunga ndoa yao” aliandika kwenye post yake aliyoituma.This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging