Google PlusRSS FeedEmail

DJ G LOVE AELEZEA TOFAUTI KATI YA DIAMOND NA ALI KIBA




BAADA ya kuwepo marumbano mbalimbali juu ya uwezo wao wa kazi katika ya wasanii wawili wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnum, Ali Kiba, hatimaye mmiliki wa G-Records, Ramadhan a’ka; DJ G-Love ameweka wazi tofauti kati ya wasanii hao wawili.

Mmiliki huyo ambaye hapo awali alishawahi kuwa msimamizi wa kazi za Ali Kiba na ndio miongoni mwa Studio zilizomtoa msanii huyo kimuziki aliweka wazi kuwa tofauti kati ya wasanii hao wawili ni kipaji na biashara.

Ambapo alieleza kuwa Ali Kiba amemzidi mwenzake kwa sababu yeye anakipaji na uwezo mkubwa wa sauti ingawa sasa Diamond ameweza kufanya mabadiliko mbalimbali ya muziki kwa kuufanya muziki kuwa ni sehemu ya biashara.

“Ukweli ni kwamba Kiba anasauti na kipaji ambapo hata siku za awali Diamond alishawahi kukiri kuwa angekuwa na sauti kama ya Ali KJiba angeweza kufanya mambo makubwa lakini Diamond ameufanya muziki kuwa ni biashra hivyo awezi kuwaangusha wanaomsimamia” alisema DJ G Love.

Kwa mujibu wa mtandao wa Vijimambo umeandika kuwa Dj G-Love ameweka bayana kuwa Diamond mbali na kuufanya muziki wake ni sehemu ya biashara pia ameweza kuajili watu wengi ambao wote wanasimamia kazi yake.

“Hata mimi nilipokuwa ninamsimamia kazi Kiba hakujua nyuma tupo wangapi lakini ni kweli nyuma sikuwa mimi peke yangu haoli hiyo ilip[elekea kazi kuisimamia vyema na ndio Diamond anachokifan ya sasa” alisema.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging