Google PlusRSS FeedEmail

POLICE MASHAKANI MARA BAADA YA KUCHEZA DANSI AKIWA AMEVALIA SARE

                

Mgogoro umeibuka nchini India baada ya polisi mwanamke nchini humo kucheza densi ukumbini na muigizaji maarufu Shah Rukh Khan katika tamasha la polisi lililofanyika katika jimbo la Bengal Magharibi.

Wanasiasa wa upinzani wamekosoa densi hiyo, wakisema afisa huyo wa polisi kucheza densi akiwa amevalia sare zake, imehujumu heshima kwa  jeshi la polisi.

Kiongozi wa jimbo la West Bengal,Mamata Banerjee, aliyehudhuria tamasha hilo, pia alishambuliwa kwa kuruhusu tamasha hilo kufanyika.

Polisi huyo mwanamke na muigizaji Shah Rukh Khan bado hawajatoa tamko lolote kuhusu sakata hiyo.

Densi hiyo, ilifanyika katika tamasha maalum la polisi lililofanyika siku ya Jumamosi.

Shah Rukh Khan ni mmoja wa waigizaji mashuhuri nchini India na duniani , na hivi maajuzi alitajwa kama balozi wa jimbo la Bengal Magharibi.

Rais wa chama cha upinzani cha Congress katika jimbo hilo, Adhir Ranjan Chowdhury , alituhumu mkuu wa jimbo hilo Bi Banerjee kwa kukiuka, katiba kwa kumruhusu afisaa hiyo kucheza densi akiwa amevalia sare yake.

"katiba hairuhusu mtu kucheza densi akiwa amevalia sare za kazi. Ni aibu tupu kwamba sifa ya idara ya polisi ilivunjiwa heshima hivyo. Kwa kuruhusu afisa wa polisi kucheza katika hali ile, alivunja katiba ya India, '' alinukuliwa akisema afisa mkuu wa upinzani jimboni humo.

Taarifa zinasema kuwa kamishna mkuu wa zamani wa polisi Nirupam Som alisema, "wakati wa muhula wangu uongozini, singeruhusu hata kidogo polisi kucheza densi kama vile. ''

Lakini baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii, walipuuza sakata hii iliyozua mgogoro huu wote kama kutokuwa kichekesho.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging