Google PlusRSS FeedEmail

TUNDAMANA AUFUATA USHAURI WA ALI KIBAMwimbaji wa Tip Top Connection, TundaMan aliwashangaza wengi baada ya kueleza kuwa alipokea simu yenye namba nyingi asizozielewa na ghafla akapata mshtuko na kuishiwa nguvu, hali iliyomsababisha akimbizwe hospitali ambapo alipewa matibabu.

Licha ya kuwa wataalam na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) walieleza wazi kuwa kitaalam simu haiwezi kabisa kuwa chanzo cha tatizo hilo, TundaMan alisisitiza kuwa yeye ndiye aliyepata tatizo na anajua kilichotokea.

“Wao wanasema haiwezekani kwa sababu hilo tatizo halikuwakuta…lakini kwa kuwa mimi ndiye nimekuwa affected kwa siku mbili tatu, mimi naamini kuwa tukio hilo lipo na limekuja baada ya kupokea ile simu. Wao wanaongea kitaalam siwezi kubishana nao, lakini mimi limenikuta na nimeona.” Aliiambia tovuti ya Times Fm.

Kutokana na sintofahamu hiyo, Tundaman ameeleza kuwa msanii mwenzake, Ali Kiba alimshauri kwenda katika nyumba ya ibada ili apate dua maalum.

“Yeah inawezekana (ni ushirikina) kwa sababu vitu kama hivyo huwa vinatokea sana na ndio maana ndugu yangu Ali Kiba amenishauri nikapate dua.” Amesema Tunda Man.

Ameeleza kuwa tayari amechukua uamuzi huo ingawa hali yake pia inaendelea kuimarika baada ya kupata matibabu. Kwa mujibu wake, Dua ndilo kimbilio lake la mwisho.
SOURCE:TIMESFM

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging