Google PlusRSS FeedEmail

BEN POL AZUA MJADALA INSTAGRAM


MWANAMUZIKI wa miondoko ya RnB Tanzania amejikuta kwenye wakati mgumu katika mitandao ya kijamii mara baada ya kupost picha ya mwimbaji wa kike Alicia Keys akiwa mtupu na mjamzito na kuandika ‘I Love it’ .

Picha hiyo imepokelewa kwa mitazamo tofauti ya mashabiki wanaomfuata Instagram ambapo wengine walionesha kushangazwa na kitendo hicho huku wengine wakimsapot na kumtetea wakieleza kuwa hakuna kosa kwa kuwa alikuwa anasapoti kampeni ya ‘We are Here’ inayopewa nguvu na Alicia kwa mtindo huo.

Kampeni hiyo inatafuta sapoti ya watu wote duniani wanaopenda dunia iwe na amani kwa ajili ya kuwalinda zaidi watoto. Alicia amefanya wimbo maalum kwa ajili ya kampeni hiyo na ameeleza kuwa anataka dunia nzima iuimbe.

“It’s you and me on a mission to create a kinder and more peaceful world. The #WeAreHere Movement begins today. Read more here and thank you @nickkristof for sharing your bright voice with all of us. (Link in bio).” Aliandika Alicia kwenye post yake aliyoweka picha hiyo.This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging