Google PlusRSS FeedEmail

LINAH KUJA KIVINGINE



MSANII wa kike nchini Linah ambaye anatamba kwa nyimbo yake aliyoifanya na muimbaji kutoka Afrika Kusini Uhuru anatarajia kuachia nyimbo mpya huku akiamini kuwa ni moja ya wimbo utakaofanya vizuri katika tasnia ya muziki.

Linah ambaye hivi sasa anafanya kazi chini ya kampuni ya kimataifa ya ‘No Fake Zone’, akizungumza na jarida hili kwa njia ya simu alisema kuwa wimbo unaofuata utakuwa mkubwa zaidi ya Ole Themba na kwamba amefanya na msanii mkubwa sana Afrika.

“Yaani inakuja kubwa zaidi ambayo hiyo itakuwa funika, waswahili wanasema itakuwa ‘ndio basi tena..’ (anacheka). Nimeshaifanya ila kuna baadhi ya vitu ambavyo naenda kumalizia. Kwa hiyo Mungu akijalia hizo wiki zinazokuja ntaenda (Afrika Kusini) kumalizia.” Alisema Linah

Hata hivyo hakumtaja msanii huyo aliyefanya nae kazi na kuahidi kuwa itakuwa surprise baada ya kazi kumalizika na kutoka kama ilivyokuwa ‘Ole Themba’.

Katika hatua nyingine, Linah ameeleza kuwa wimbo wake Ole Themba umempa mafanikio makubwa ambayo hakuwahi kuyafikia na kwamba sio Tanzania tu bali Afrika kwa ujumla kwa kuwa video yake imechezwa katika vituo vingi sana vikubwa.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging