Google PlusRSS FeedEmail

HAMZA KALALA KUFANYA COLLABO NA YAMOTO BAND

Mwimbaji mkongwe Hamza Kalala anatarajia kufanya collabo na Yamoto Band inayoundwa na vijana wenye umri mdogo walio chini ya Mkubwa na Wanae.

Mzee Kalala ameeleza kuwa ameamua kushirikiana na Yamoto Band inayoongozwa na Dogo Asley kwa kuwa ameona uwezo wao na wao wameonesha nia ya kutaka kushirikiana nae.

Katika hatua nyingine, Hamza Kalala ametangaza kuihama band yake na kujiunga na Utalii Band kwa lengo la kujikita katika kuhamasisha utalii nchini na kwamba ameachana na mpango wa kuendelea kuimba nyimbo za mapenzi.

Ameeleza kuwa Utalii Band inaweza kuwa band ya mwisho kujiunga nayo katika safari ya muziki wake wa muziki kabla hajaamua kustaafu.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging