Google PlusRSS FeedEmail

SABABU YA NICKI MINAJ KUZUILIWA KUINGIA KATIKA SHULE ALIYOSOMA YAWEKWA WAZI

Ijumaa iliyopita, Nicki Minaj aliandika malalamiko yake kwenye akaunti yake ya Twittter akidai kuwa mkuu mpya wa shule aliyosoma alimzuia kuingia shuleni hapo kuongea na wanafunzi kwa lengo la kuwainspire.

Wengi walidhani kuwa tatizo ni video na picha zisizo na maadili za Nicki Minaj ambazo zilimfanya mwalimu huyo kudhani asingekuwa mfano mzuri kwa wanafunzi wake.

Lakini kwa mujibu wa Mediatakeout, moja kati ya wajumbe wa baraza la wazazi waliweka wazi sababu ya Nicki kunyimwa kibali.

Ameeleza kuwa Nicki Minaj alilenga katika kutaka kujitangaza zaidi kwa kuwa baada ya kukatazwa na kitengo cha elimu cha New York kuingia na wapiga picha za video kwenye shule hiyo.

“Ukweli ni kwamba Ms. Minaj aliambiwa na kitengo cha elimu cha New York (NYC Department of Education) kuwa asingeruhusiwa kuingia shuleni pale na crew ya television. Kitengo hicho kina sera zake kulinda faragha na usalama wa kila mwanafunzi. Nina uhakika wote tunakubali utekelezwaji makini wa sera hii kwa kuzingatia usalama wa watoto wetu.

Ameongeza kuwa Nicki Minaj alitaka kuweka kwenye video kila kitakachofanyika pale kama sehemu ya kampeni ya kujitangaza kwa umma kwa mazuri anayofanya.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging