Google PlusRSS FeedEmail

MAN WALTER KUFANYA KAZI NA 20 PERCENT

MTAYARISHAJI wa muziki wa kizazi kipya nchini anayejulikana kwa jina la Man Walter, aliwahi kutangaza kumaliza tofauti kati yake na 20 Percent ambaye aliwahi kuwa mmoja wa watu walioifanya naye kazi ambazo zilimsababisha kunyakua tuzo 5 za Kilimanjaro aelezea mpango wa kufanya mradi mpya pamoja.

Ambapo Man Walter yupo katika maandalizi ya kufanya kazi kwa pamoja na msanii huyo anayeamini kuwa ataendelea kufanya vizuri katika tasnia ya muziki nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Man Water alielezea mipango yao na kueleza walipofikia baada ya ukimya wa muda mrefu tangu walipotangaza hatua hiyo.

“Off Course kwa sasa siwezi kuongelea sana kwa sababu wazo lilienda vizuri lakini nadhani kuna vitu viwili vitatu vilikwama, sijapata tena mawasiliano mazuri na 20. Labda tuvute subira tu, kwa sababu kama watu wana lengo la kufanya jema litakuwa tu…nadhani tuvute subira kwake.” Alisema Man Walter.

Amefafanua kuwa milango iko wazi kwa 20 Percent kufanya kazi kwake kwa kuwa yeye ni mfanyabiashara lakini pia anasubiri sana kufanya kazi na msanii huyo ili kuwahakikishia watu kuwa hakuna tatizo lolote kati yao.

20 Percent aliwahi kuchukua tuzo 5 katika kinyang’anyiro cha KTMA kwa kazi alizofanya na Man Walter.

Man Walter ameachia wimbo mpya hivi karibuni aliofanya mwenyewe kwa kushirikiana na Mbatizaji. Unaitwa ‘Wife Material’.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging