Google PlusRSS FeedEmail

BAADA YA KUNYAKUA MILIONI 50 - MWANAFAA AUAMUA KUHAMIA DAR

Mshindi wa shindano la kusaka vipaji la lillojulikana kwa jina la Tanzania Movie Talent (TMT) Mwanaafa Mwinzago, msanii huyo ambaye kwa sasa anaishi jijini Dar es Salaam baada ya kujinyakulia milioni 50, anasema kuwa anafanya mipango ya kusoma Dar es Salaam na si Mtwara tena.

“Nilirudi Mtwara kwa ajili ya kufanya mtihani wangu wa darasa la saba, na nimerudi Dar tena kwa ajili ya kurekodi filamu ya Tmt Movie, siwezi tena kurudi Mtwara nitasoma hapahapa tu,”anasema Mwanaafa.

Mwanaafa anasema kuwa kampuni ya Proin Promotions imemjengea mazingira mazuri ya kuishi kama nyota hivyo hata kama anapasi mtihani wake atahamia hapa kwani kazi ya kurekodi filamu ambayo ndio kazi anayoamini si rahisi kuifanya Mtwara, filamu ya Tmt movie imeanza kurekodiwa na kinara ni Mwanaafa.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging