Google PlusRSS FeedEmail

HASHIM LUNDENGA AKANUSHA HABARI ZA SITTI MTEMVU aka MISS TANZANIA KUJIVUA TAJI.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga (kati pichani), amekanusha uvumi uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii mapema leo, kuwa Sitti Abbas Mtemvu  amelazimika kuvua taji la Uremo la Tanzania (Redd’s Miss Tanzania 2014).

Uvumi wa Sitti kuvua taji hilo umetokana na taarifa zilizotolewa kupitia  Facebook mrembo huyo anayelalamikiwa kughushi vyeti vya kuzaliwa, akisema kutokana na vidole vya lawama anavyooshewa kiasi cha kuosa amani, amelazimika kuvua taji ili awe huru. “Habari za jioni Watanzania wenzangu, kutokana na kuwa nimekuwa nikisemwa sana, maneno mengi yasio na tija juu ya hili taji la U-Miss anzania 2014,,mpaka kupelekea nisiwe na amani na uhuru ndani ya nchi yangu Tanzania, kwa roho safi nimeamua mwenyewe kujivua taji hilo na kuacha wanaye ona anastahili taji hili apewe ili niendelee na maisha yangu kwa amani ,isiwe shida sana kwani sitegemei taji hili ili kuishi!!” imeandikwa katika ukurasa huo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging