Msanii huyo amekamatwa leo mchana akiwa katika sehemu ya kuondokea ambapo alifanyiwa uchunguzi katika maungo yake na kukamatwa na kete 14 alizokuwa ameweka katika mfuko wa shati lake na misokoto miwili ya bangi na vifaa vingine vinavyohusisha na masuala ya uvutaji dawa za kulevya.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamishina Msaidizi wa Polisi ambaye pia ni kamanda wa Viwanda vya ndege Tanzania Hamisi Selemani alieleza kuwa msanii huyo alikiri kuwa dawa hizo ni za kwake na kwamba anatumia dawa hizo.







