Google PlusRSS FeedEmail

CHID BENZ AJIKUTA KATIKA WAKATI MGUMU MAHAKAMANI

Msanii wa muziki wa hip hop nchini, Rashid Makwaro ‘Chid Benz’ jana alizuiwa na askari kuingia ndani ya chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa sababu ya mavazi na mapambo yake mwilini.


Chid Benz alifika mahakamani hapo kusikiliza kesi yake lakini kutokana na mavazi aliyovaa, mapambo na kipini puani alijikuta akizuiwa. Aliwasili mahakamani hapo asubuhi ili kusikiliza kesi yake inayomkabili ya kukutwa na dawa za kulevya iliyokuwa itajwe mbele ya Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema.

Lakini, wakati akitaka kuingia ndani ya chumba cha mahakama, askari aliyekuwa mlangoni alimtaka apandishe suruali yake aliyokuwa ameivaa mtindo wa mlegezo na afunge vishikizo vya shati lake ili kuificha cheni ya kiasili aliyokuwa ameivaa shingoni.


Mbali na hayo, askari huyo alimtaka Chid Benz pia avue miwani aliyokuwa ameiva na kipini kilichokuwa kikining’inia puani na baada ya kukamilisha utaratibu huo aliruhusiwa kuingia mahakamani kwa ajili ya kuendelea kusikiliza kesi yake.


Baada ya msanii huyo kuingia mahakamani, mawakili wa Serikali, Ofmed Mtenga na Leonard Challo waliomba kesi hiyo iahirishwe kwa madai kuwa upelelezi wake bado haujakamilika, wakiomba ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa. Hakimu Lema alikubaliana na maelezo hayo na kuiahirisha kesi hiyo hadi Desemba Mosi kwa ajili ya kuangalia kama upelelezi wake utakuwa umekamilika au la.


Awali, Chid Benz alitishia kuwapiga wapigapicha huku akitoa maneno makali dhidi yao, lakini mama yake aliwaomba wasimpige picha kijana mwenzao, lakini askari walimweleza mama huyo kuwa waandishi hao wapo kazini, waachwe wafanye kazi yao.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging