Napenda kumwambia mdogo wangu Q Chillah huku siyo kama katika muziki, huku tunavaa kulinga na uhusika, siyo kuvaa tu ilimradi umevaa tu, maskini hawezi kuvaa suti, au mchungaji kuvaa pensi au kuonekana tofauti na hadithi inavyosema,”anasema Dude.
Dude aliyasema hayo kufuatia kauli ambayo iliwahi kutolewa na msanii huyo wa muziki na filamu kuwa wasanii wengi wa filamu hawajipangi katika mavazi, wakati yeye anapoingia katika sinema yoyote anajipanga na kununua nguo za kutosha hadi milioni kwa ajili ya filamu anayoigiza.
“Namkumbusha Q Chillah huku kugumu kuliko kwenye muziki anakotaka kukimbia tunavaa kulinga na uhusika hatavai ilimradi tu umevaa, ubora wa uigizaji wako utaonekana kwa mashabiki zako hakuna ubishoo katika kuigiza,”
Huu ni mpambano wa aina yake kati ya Dude na Q Chillah ambaye anayejiita Majid Michael kwa sasa kwani matarajio yake ni kuwa mwigizaji wa kimataifa na kwa kipaji chake Q Chillah alianza kuigiza akiwa na kundi la Mzimuni linaloongozwa na Jimmy Master na baadae kujikita katika muziki.