MWIGIZAJI mkongwe katika tasnia ya filamu Cath Rupia amefunguka kwa kusema kuwa makundi kwa sasa hayana msaada wowote kwa msanii zaidi ya mtu mwenyewe kufanya kazi kwa juhudi zake binafsi kwani hakuna anayeweza kumsaidia msanii mwenzake kwa ajili ya kufanikisha kazi.
“Ukiona msanii au mtayarishaji wa filamu amefanikiwa kutoa sinema yake na kuingia mtaani ujue amehangaika mwenyewe kutafuta mtaji na kutengeneza kazi yake, pamoja kuwa kuna makundi kama Bongo Movie na mengineyo hakuna kitu,”anasema Cath.
Msanii huyo anasema kuwa kwa sasa kuna changamoto nyingi kwa mtayarishaji wa filamu ikiwa pamoja na gharama kubwa za vibali, malipo ya TRA huku maharamia nao wanazidi kujinuifaisha huku hali ya wasanii ikizidi kuwa mbaya kila kukicha kwani hakuna maslahi ya kazi yao.