
MWIGIZAJI wa kike wa filamu Bongo Irene Uwoya ametamba kwa kusema kuwa anafunga mwaka kwa kuwa mtayarishaji mkubwa wa filamu aliyetengeneza filamu ya kufunga mwaka gharama kubwa na kushirikisha wasanii wakubwa kutoka Afrika ya Kusini na uturuki, filamu yake ya Kisoda.
“Najaribu kutoka kimataifa kwa kutengeneza filamu kubwa na yenye wasanii wa kimataifa filamu yangu ya Kisoda itatutoa kimasomaso wabongo, sikuangalia gharama bali ni kulitangaza Taifa langu katika Nyanja za filamu, itapendwa Uturuki na Afrika ya kusini pia,”anasema Irene
Filamu ya Kisoda imerekodiwa nchini Ututruki kwa asilimia kama 9 hivi na asilimia zilizobaki zote ni nchini Afrika ya Kusini, ikiwashirikisha King Majuto, wasanii wawili kutoka THT, Mariam Ismail na wasanii kutoka Afrika ya Kusini na Uturuki anasema ndio filamu itakayotambulisha kampuni yake ya Apple Entertainment 2015.