MUONGOZAJI wa filamu William J. Mtitu amesema kuwa hawatakuwa tayari kuua familia zao kwa kukosa mahitaji kufuatia kampuni ya Steps Entertainment kushusha bei ya filamu kutoka 3000 hadi 1500 kwani hizo ni hila za wazi kuua kampuni nyingine ndogo ndogo ili wabaki pekee yao.
“Ndugu yangu maisha kila siku yanapanda mkate wenye umefikia 3,000 sasa inatushangaza kuwa anatokea mtu mmoja mwenye fedha zake anataka kuua familia za watanzania wanaojishughulisha na kazi za kusambaza filamu kwa kushusha bei si ana mpango wa kutuua huyo, hatutokubali,”anasema Mtitu.
Mtitu anasema kuwa historia inaonyesha kuwa toka kuingia kwa kampuni hiyo katika usambazaji ni kampuni nyingi zimekufa baada kila msimu kampuni hiyo kushusha bei na hali hiyo inaendelea, moja ya sababu kubwa ya kushusha bei inasemekana kutokana na maharamia kutawala soko hilo na kushundwa kushughulikiwa.