Google PlusRSS FeedEmail

JAMAL ACHIA KITU KIPYA SOKONI

FILAMU ya Jamal iliyotengenezwa na mtayarishaji Fike Wilson imeingia leo sokoni kwa kishindo na kupokelewa na wadau wa filamu nchini kote, filamu hiyo ambayo ni ya mapigano ikishiriki wasanii mahiri katika filamu za mapigano, ikiwa na sehemu ya 3 na 4.

“Filamu ya Jamal ni daraja la historia ya maisha ya kila siku la inaelezewa kwa aina tofauti na vile tulivyozoea, kuna upinzani wa kweli watu wanaonyesha vipaji halisi, hapa kuna J Plus, Kisinini huku mwenyewe nikiongoza jahazi, ni kazi nzuri,”anasema Fike.

Chrispin Kisinini ndiye adui mkuu huku ikiwa imewashirikisha wasanii nyota kama Hamed Olotu, Mc Kenyatta, Mobi Mpambala na Wasanii wengi chipukizi wanaoibukia Katika Sanaa ya Filamu Bongo.

Kwa upande wa uongozaji imeongozwa na Sameer Srivastava wa muandishi wa filamu hiyo ni Fike Wilson, Filamu ya JAMAL imebeba ujumbe masuala ya kifamilia na mapenzi Kwa ujumla mchezo wa Ndondi umetumika kama daraja la kufikisha ujumbe Kwa jamii ni filamu yenye mchanganyiko wa Action & Drama.

Inasambazwa na kampuni ya Pilipili Entertainment ya jijini Dar es Salaam na inapatikana nchi nzima nunua nakala halisi kuwainua wasanii na si kununua kazi bandia

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging