

“Mwanangu nakwambia umaarufu ni shida kubwa, zamani nikirudi nyumbani Bukoba nilikuwa nina amani kwani hakuna hata aliyeniona kama ni mtu maarufu, lakini baada ya kifo cha Kanumba na mimi kuingia kuigiza na watu kunijua ni shida,”anasema Mama Kanumba.
Mama Kanumba anasema kuwa hivi karibuni alifiwa na kwenda msibani Bukoba, alijikuta katika wakati mgumu kwani kila kitu alikuwa akisakiziwa yeye kwa sababu tu ameonekana katika filamu na wanaamini kuwa anapesa nyingi, hivyo inapofikia suala kutoa fedha au kununua chochote anaangaliwa yeye...