Google PlusRSS FeedEmail

MLELA APANGA KUFUNGA NDOA MWAKA HUU

                                  
Mwigizaji wa filamu za Kibongo, Yusuf Mlela amefunguka kwamba baada ya kuishi ‘singo’ kwa muda mrefu, sasa anajipanga kuoa hivyo ndani ya mwaka huu lazima ndoto yake hiyo itimie.

Mlela alisema mwaka huu amejiwekea malengo mengi lakini kubwa zaidi ni kuoa kwani anahisi akiendelea kuwa peke yake kuna mambo atakwama kwa kuwa hatakuwa na mtu wa kumshauri kwa karibu.

“Kiukweli maisha yenyewe ni mafupi na umri nao unaenda hivyo lengo langu kubwa kwa mwaka huu ni kuoa na kuhusu nitamuoa nani itajulikana baadaye lakini kwa sasa tambueni kwamba mwaka huu lazima nioe, nimechoka maisha ya ubachela,” alisema Mlela.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging