Google PlusRSS FeedEmail

SINGLE MTAMBALIKE ATAMANI KUWA MKULIMA

        Single Mtambalike
SINGLE Mtambalike ‘Ritchie’ amedai kuwa soko la filamu kwa sasa ni gumu sana na si la kufanya mchezo kwani kama kuna msanii au mtayarishaji ambaye hajajipanga na sehemu gani ya kupeleka kuuza basi unaweza kujikuta unapoteza muda wako na pesa pia kushindwa kuwafikia watu.


“Soko letu linabana sana kama hauna shughuli nyingine kichwa kinawaka moto, nimetoa filamu yangu ya Msala nimewapa zawadi watanzania nataka ifike popote ndio maana nimwapa hawa jamaa wasambaze nimerudisha mpira kwa kipa,”anasema Ritchie

Ritchie anasema kuwa filamu yake ya Msala inafungua mwaka angependa kila mtu aipate lakini anasema hali ya soko itaendelea katika hali kama hii basi ataacha na uigizaji na kuingia katika kilimo rasmi yupo katika maandalizi ya kuwa mfugaji na mkulima lakini sio kama anaacha kuigiza.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging