Google PlusRSS FeedEmail

TWEET ZA DAVIDO HAZIKUWA ZIKIMLENGA DIAMOND

                                  
Mitandao mikubwa ya Nigeria ikiwemo Pulse na News24 imeandika kuwa tweets hizo ambazo Davido anamzungumzia mtu asiye na shukrani kwake na kwamba kiama chake kinakuja, zimemlenga Diamond.

Uhusiano kati ya mastaa hao wawili uliingia dosari siku ya fainali ya shindano la Big Brother Africa ambapo baada ya Idris kushinda Davido alitweet ‘And They Cheat Again’ na Diamond ambaye usiku huo alishinda tuzo ya TFA za Nigeria aliijibu kwa ujumbe wa kuibeza.

Kufuatia tweet hiyo ya Davido, watanzania wengi walimshambulia kwa matusi na kumtaka aombe radhi kitu ambacho aligoma kufanya.

Tangu hapo, kumekuwepo na  maneno kuwa  uhusiano kati ya wawili hao umevunjika na ndio maana imekuwa rahisi kwa wengi kuhusu tweet hizo  zilizokuwa zikimlenga Diamond.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging