Google PlusRSS FeedEmail

HII NDIO TAARIFA RASMI KUHUSIANA NA AFYA YA BOBBI KRISTINABado kuna utata kuhusu kinaachoendelea juu ya afya ya Bobbi Kristina, mtoto wa pekee wa Marehemu Whitney Houston, mengi yanaendelea kuzungumzwa kuhusu hali yake huku wengine wakisema kuwa leo ni siku ambayo familia hiyo imeruhusu madaktari kumtoa mashine ya kupumulia ambayo aliwekewa toka siku ambayo alifikishwa hospitali baada ya kukutwa akiwa ameanguka ndani ya bafu, Georgia Marekani.

Baada ya yote kusikika familia ya Bobbi huyo imeamua kutumia kampuni ya wanasheria wao kutoa maelezo rasmi kuhusu kila ambacho kimesikika kuhusu hali ya mtoto huyo, taarifa hiyo imekanusha uvumi wote uliowahi kusikika ikiwemo ishu ya kumtoa mipira ya kupumulia siku ya leo ambapo ni siku ambayo mama yake alifariki.

Katika taarifa hiyo ya Wanasheria wa familia hiyo wamesema wanaangalia namna ya kuwachukulia hatu wote waliotoa taarifa za uongo ikiwemo waliosema walizungumza na wahusika wa familia hiyo kitu ambacho sio kweli.

Bado hakuna taarifa rasmi ambayo familia hiyo imetoa kuhusu hali ya mtoto huyo, leo inatimia miaka miaka mitatu tangu afariki Whitney Houston ambaye alikutwa pia ameanguka bafuni.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging