JIMMY Mafufu mtayarishaji na mwigizaji wa filamu amefunguka kwa kuweka wazi kama alikuwa ni mtumiaji wa bangi na pombe lakini anashukuru Mungu ameacha kutumia vilevi hivho sambamba nkwani ni Mjukuu wa Askofu Asumwisye Mwaisabila.
“Toka niache kuvuta sigara nina mwezi mmoja nilianza kuacha pombe nikaacha kuvuta Bangi, nakupa ushuhuda unajua mimi ni mjukuu wa Askofu Asumwisye Mwaisabila mwalimu wa watu wa Mungu,”anasema Jimmy.
Jimmy ambaye hajabaisha Babu yake ni baba Askofu wa Kanisa gani? Amedai kuwa ameamua kutoa ushuhuda kwani toka kuoa kwake amebadilika sana kitabia hata anafikiria siku akiacha kuigiza atakuwa mchungaji ni vema akajiandaa mapema na kuwa mwadilifu katika jamii, huku alikopita anasema ilikuwa ujana tu.