Google PlusRSS FeedEmail

KAMA KAWA SHILOLE NA NUHU

                                

MWIGIZAJI na mwanamuziki wa kizazi kipya Zuwena Mohamed  - Shilole kweli anaweza kulea na kama unabisha basi kutana na kijana aliyebarikiwa kushusha mlima wa Kitonga bila jasho anatikisa tu kwa shishi baby anajulikana kwa jina la Nuhu Mziwanda yupo vizuri katika sekta hiyo.


Kijana anajaribu kuuonyesha umma kuwa mapenzi ni pamoja na kula mbata mwanzo mwisho huku ukipangiwa hata kubarizi eti kisa una mwanamke unayempenda lakini yeye hakupendi, kama anakupenda kwa dhati anakuchapaje vibao hadharani?

       

“Mwanaume rijali aliyekamilika hampigi mpenzi wake wala kumrudishia kibao au kofi alilopigwa na mpenzi wake, naamini kwenye mapenzi ya kweli wivu lazima na kugombana kwenye mapenzi kama kwenda chooni, nipige nikome mkewe wangu,”Mziwanda.

Maneno hayo aliyoongea King’asti wa Shishi ni ya kujidhalilisha kwani mwanaume mwenye maamuzi na anayewajibika kwa ajili ya familia yake hawezi kujivua hivyo maneno hayo alitakiwa kuwaeleza watu wasiojua maisha yao ya purukushani kila kukicha, sijuia kama mchizi ana familia kweli!

Kama kuna chama cha kutetea na kuwajengea akili wanaume walio katika mahusiano ya kimapenzi wamsaidie kijana ni mgonjwa tayari ameathirika kisaiklojia kukubali kuwa House Boy kwa sababu tu analelewa na kuwahadaa watu eti mapenzi, ni hatari kwa staili hiyo kusikia vijana wakiolewa si ajabu.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging