Google PlusRSS FeedEmail

KANUMBA THE GREAT FILMS HAIJAFUNGWA- NOVA

                  

PRODUCTION Manager wa kampuni ya marehemu Steven Kanumba Kanumba The Great Films Novatus Mayenja ‘Nova’ amefunguka kwa kukanusha kuwa kampuni hiyo imefilisika bali imehamishwa kutoka mitaa ya Sinza na kurudishwa nyumbani mitaa ya Kimara Temboni.

“Kampuni ipo kama kawaida isipokuwa tu, utaratibu umebadilika kwa kuhamisha ofisi kutoka ilipokuwa na kuhamishia nyumbani kwa mama Kanumba na kazi zinaendelea kama kawaida,”anasema Nova.
              Frola Mtegoa
Nova amedai kuwa tatizo lilikuwa ni kodi kwani kodi imekuwa ikipanda kila mwaka hivyo walimudu kulipa kwa miaka miwili kwa pamoja wakaona haina sababu kulipa kodi kubwa bila sababu ya msingi waktai wanaweza kufanya kazi popote.

Hivi karibuni kuna minong’ono ambayo imekuwa ikisikika kuwa moja ya sababu ya kampuni hiyo kudorora ni mama mzazi wa marehemu kuingilia kufanya kazi ambazo hana ujuzi nazo, jambo ambalo limewafanya wasaidizi wake wakimbie na kuiacha kampuni hiyo ifie mikononi mwake.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging